TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA UDEREVA

Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) Mradi wa Kilwa unakaribisha maombi ya kazi ya udereva kwa  watanzania wenye sifa , Vigezo na uwezo wa kujaza nafasi 1 (moja) kama inavyoonesha katika tangazo hili.

 

 1. SIFA ZA MWOMBAJI

i)Mwombaji awe ni raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 30 na umri usiozidi miaka 45.

 1. ii) Dereva Daraja la II
 2. Mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la C, C1, C2 au C3 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua miaka 5.

iii) Mwombaji awe amefuzu mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

 1. iv) Mwombaji mwenye Cheti cha Ufundi Level II na Grade II na au wenye cheti cha NIT watafikiriwa kwanza.

 

 1. MAJUKUMU YA KAZI
 2. i) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
 3. ii) Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

iii) Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.

 1. iv) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali maeneo ya mradi.
 2. v) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (LogBook).
 3. vi) Kufanya usafi wa gari

vii) Kutotumia au kuendesha gari la mradi bila ruhusa ya Msimamizi wa Kazi

Viii)Kufuata sheria na taratibu zote za usalama barabarani kwa mujibu wa sheria na taratibu za Tanzania

iXi) Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekezwa na Msimamizi wake.

 

 1. MASHARTI YA JUMLA
 2. i) Waombaji wote waambananishe maombi ya kazi na cheti cha kuzaliwa.
 3. ii) Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika majina yao kamili, Pamoja na Majina ya wadhamini wawili na anuani/simu zao.

 

iii)

 1. iv) Maombi yaambatane na Vyeti vya kitaaluma
 2. v) Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
 3. vi) Mwombaji mwenye sifa na anajua maeneo ya mradi (Kilwa) atafikiriwa kwanza

 

 

Maombi yote ya kazi yatumwe kwa anuani ifuatayo:

 

Mkuu wa Mradi

TCRS Kilwa

P.O. Box 62,

Kilwa-Lindi

tcrskilwa2017@gmail.com

 

Mwisho wa kutuma maombi ni Jumanne ya tarehe 11/10/2022 saa kumi jioni.

 

Waombaji ambao hawataitwa kwenye usaili wajue kwamba hawakuchaguliwa kwa ajili usaili.

Apply for this position

Allowed Type(s): .pdf, .doc, .docx