TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA UDEREVA

October 3, 2022
admin

15/09/2022

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA UDEREVA
Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) Mradi wa Kilwa unakaribisha maombi ya kazi ya udereva kwa watanzania wenye sifa , Vigezo na uwezo wa kujaza nafasi 1 (moja) kama inavyoonesha katika tangazo hili.

  1. SIFA ZA MWOMBAJI
    i) Mwombaji awe ni raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 30 na umri usiozidi miaka 45.
    ii) Dereva Daraja la II
    ii. Mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la C, C1, C2 au C3 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua miaka 5.
    iii) Mwombaji awe amefuzu mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
    iv) Mwombaji mwenye Cheti cha Ufundi Level II na Grade II na au wenye cheti cha NIT watafikiriwa kwanza.
  2. MAJUKUMU YA KAZI
    i) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
    ii) Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
    iii) Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
    iv) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali maeneo ya mradi.
    v) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (LogBook).
    vi) Kufanya usafi wa gari
    vii) Kutotumia au kuendesha gari la mradi bila ruhusa ya Msimamizi wa Kazi
    Viii)Kufuata sheria na taratibu zote za usalama barabarani kwa mujibu wa sheria na taratibu za Tanzania
    iXi) Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekezwa na Msimamizi wake.
  3. MASHARTI YA JUMLA
    i) Waombaji wote waambananishe maombi ya kazi na cheti cha kuzaliwa.
    ii) Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika majina yao kamili, Pamoja na Majina ya wadhamini wawili na anuani/simu zao.

iii)
iv) Maombi yaambatane na Vyeti vya kitaaluma
v) Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi) Mwombaji mwenye sifa na anajua maeneo ya mradi (Kilwa) atafikiriwa kwanza

Maombi yote ya kazi yatumwe kwa anuani ifuatayo:

Mkuu wa Mradi
TCRS Kilwa
P.O. Box 62,
Kilwa-Lindi
tcrskilwa2017@gmail.com

Mwisho wa kutuma maombi ni Jumanne ya tarehe 20/09/2022 saa kumi jioni.

Waombaji ambao hawataitwa kwenye usaili wajue kwamba hawakuchaguliwa kwa ajili usaili.

Job Category: TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA UDEREVA
Job Type: Full Time
Job Location: Kilwa

Apply for this position

Allowed Type(s): .pdf, .doc, .docx